Date: 
09-08-2022
Reading: 
Mathayo 6:31-34

Jumanne asubuhi tarehe 09.08.2022

Mathayo 6:31-34

[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Mlango wa kuingia mbinguni;

Yesu anaendelea na mafundisho au hotuba ya mlimani akielezea kutosumbuka. Anafundisha juu kutosumbukia kula, kunywa na kuvaa maana Bwana huyajua mahitaji yote. Yesu hakumaanisha watu wasitafute chakula na mavazi, bali katika yote wamtangulize na kumtegemea Bwana.

Yesu anatufundisha kuutafuta kwanza ufalme wake, na mengine yote tutazidishiwa. Maana yake, tumjue Kristo kwanza, ndipo tufanye mambo yote kwa Utukufu wake. Tukimjua Yesu na kumtumikia kwa uaminifu atatuonesha mlango wa kuingia mbinguni.

Siku njema.