Event Date: 
12-08-2022

Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral mnamo tarehe 19/3/2022 walikutana usharikani kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Umoja huo kwa mwaka 2022. Katika mkutano huo wanawake waliweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo na kanisa kwa ujumla.

Mkutano huo mkuu wa mwaka ulifunguliwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Mch Charles Mzinga ambaye katika salaam zake aliwataka washiriki kujadili kwa urefu na kutafuta suluhu juu ya chagamoto mbalimbali zinazoukabili umoja huo ili uweze kuimarika zaidi kwa maslahi mapana ya wanawake wa usharika na kanisa kwa ujumla.

--------------------

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral uliofanuyika usharikani tarehe, 19 Machi 2022.