MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 28 MEI, 2023
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI ROHO MTAKATIFU MSAADA WETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakunamgenialiyetufikiakwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 21/05/2023
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
6. Uongozi wa Wagane na Wajane unapenda kuwatangazia Wajane wote kwamba kutakuwa na Kongamano la Wajane la nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki litakalofanyika Chuo Kikuu Cha Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 27 mwezi wa nane 2023. Wajane wote mnaweza kuonana na Uongozi ili kupata maelekezo zaidi.
7. Leo tarehe 28/05/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika Karibuni.
8. Uongozi wa kwaya ya Umoja unapenda kuwatangazia vikundi vyote na washarika waliotayari kujiunga na kwaya ya umoja kushiriki mazoezi ya uimbaji wa Reformation kila siku ya Jumanne saa 11:00 jioni.
8. Shukrani. Familia ya Edith Mashasi watamtolea Mungu shukrani ya pekee kwaajili ya mambo makuu ambayo Mungu amewatendea katika familia, pia kwaajili ya maisha ya wazazi wao ikiwa ni pamoja na Mungu kuwapigania katika afya zao. Shukrani hii itakayofanyika jumapili ya tarehe 04.06.2023 katika ibada ya tatu Neno.1wathesalinike 5:18 Wimbo 358 TMW, kwaya kuu : Nitayainua Macho yangu.
9. Kesho jumatatu tarehe 29/05/2023 saa 11.00 jioni kutakuwa na Ibada ya kuenea kwa Roho Mtakatifu. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Kwanza.
10. Jumapili ijayo tarehe 04/06/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
11. Uongozi wa usharika unapenda kuwatangazia wazazi wa watoto wa shule ya jumapili kuwa tarehe 14-15/06/2023 kutakuwa na kambi ya watoto hapa usharikani muda ni saa 02.30 asubuhi hadi 10:00 jioni masomo yatakayofundishwa ni
- Afya, mazingira na ukuaji
- Haki za watoto , wajibu wa watoto
- Kufahamu na kupinga ukatili
- Upendo na msamaha
- Watoto na utandawazi
Na tarehe 17.06.2023 watakwenda usharika wa kitunda relini kuhitimisha mafunzo hayo katika ngazi ya jimbo, kwaajili hiyo tunaomba ushirirkiano wenu wazazi na kuwahimiza watoto kuja kujifunza.
12. NDOA. HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbayna Masaki: KWA MAMA UPHOO SWAI
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, MakongonaUbungo:
KWA BW & BI CHARLES LYIMO
- Ilala, Chang’ombenaBuguruni: KWA MR & MRS RWEIKIZA
- Kinondoni: BW & BI DR T.M ONESMO
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: - BW JOSEPH & BI VUPE MPUYA
- Upanga:KWA MR & MRS SIMBO NKYA
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: KWA MAMA FOIBE KIDA
- English Service: KWA FAMILIA YA KISONGO
14. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi
laKwanza