Event Date: 
22-10-2023

Siku ya Jumapili, tarehe 22/10/2023, KKKT -DMP Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ulifanya maadhimisho ya kilele cha sikukuu ya mavuno ya mwaka 2023, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa washarika kumtolea Mungu sehemu ya matunda au mavuno ya kazi walizozifanya kwa kipindi cha mwaka mzima.

Ibada ya kusherehekea sikukuu hii ya mavuno kwa mwaka huu imefanyika katika viwanja vya usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral huku ikihudhuiriwa na mamia ya washarika waliojitokeza kwa wingi wakiwa na mavuno yao tayari kwa kumtolea Mungu.

Ibada hiyo imeongozwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza, akiambatana na Mchungaji Kiongozi wa Usharika Chaplain Charles Mzinga, Mchungaji Joseph Mlaki na Mchungaji Gwakisa Mwipopo; wakisaidiwa na Watumishi wote wa Usharika pamoja na Wazee wa Kanisa.

Akizungumza wakati wa Ibada hiyo, Dean Chediel Lwiza aliwakumbusha washarika wa Azania Front Cathedral kuwa na imani na kujenga utamaduni wa kumtolea Mungu sadaka hususani ile ya mavuno kama ambavyo yanaeleza maaandiko matakatifu.

Sisi washarika wa Usharika wa Kanisa Kuu tunapokuja kwenye mavuno, tunakuja kwenye sikukuu kamili ya kanisa ya utoaji. SIKUKUU KAMILI YA KANISA YA UTOAJI”. alisema Dean Chediel Lwiza.

“Imani inajenga ufahamu wako kuhusu kitu ambacho Mungu alitenda, kitu ambacho Mungu anatenda na kitu ambacho Mungu atatenda”. 

“Inawezekana ndugu wasijue, marafiki wasijue, na wazazi wasijue lakini madam ilitolewa kwa jili hiyo, basi itaishi. Na siku moja, watoto wake, uzao wake, kizazi chake kitakapokuwa kimesimama ile SADAKA itasema maneno ya Baba, maneno yam toto nimeyatakabali, yaani nimeyasikia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, nikayaelewa, nikayapima kiroho, nikayapima kimwili, nikayapima kimaisha, nikaona naam nimeyatakabali (kuyakubali kama yalivyo), alisema Dean Chediel Lwiza .

Ibada ya sikukuu ya mavuno katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral imehudhuriwa na mamia ya washarika waliokuwa na shauku kubwa ya kumtolea Mungu sadaka hiyo. Ibada ya mavuno ilitanguliwa na maandamano mafupi na utoaji wa sadaka pamoja na mavuno huku ikihitimishwa kwa mahubiri kutoka kwa Dean Chediel Lwiza na mwisho kabisa ukifanyika mnada wa bidhaa au mavuno yaliyokuwa yamewasilishwa na washarika.

Pia Kwaya ya Ukombozi kutoka Usharika wa KKKT Msasani iliungana na Kwaya za Usharika wa Azania Front Cathedral katika kuipamba ibada hiyo kupitia tungo mbalimbali za kumtukuza Bwana wetu.

------------------------------

Neno Kuu Lililotumika: MWANZO 4:4B

BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake.

 

KUTOKA 3:1 -3

1 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa niende nione kioja hiki, kwa nini kichaka hiki hakiteketei. ...................

 

ZABURI 39: 1 -7

1 Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu. 2 Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya, Sina faraja, maumivu yangu yakazidi. 3 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; Nilisema kwa ulimi wangu, 4 BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na idadi ya siku zangu ni ngapi; Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi. 5 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili. 6 Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi. 7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako.

 

MATENDO 9:1 -9

1 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3 Wakati alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa? 5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa. 6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, waliisikia sauti, lakini hawakuona mtu. 8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

 

Tazama AZFTV: Ibada ya Mavuno 2023