MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 10 DISEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA 2 KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

YESU ANAKUJA KATIKA UTUKUFU WAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 03/12/2023

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Usharika unapenda kuwatangazia Wazazi na Walezi kuwaandikisha watoto wa Kipaimara Mwaka wa Kwanza 2024 katika ofisi ya Parish Worker Umri ni kuanzia miaka 12.  

SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 17/12/2023

IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  • Familia ya Mary Msuya watamshukuru Mungu kwa mema yote aliyowajalia pamoja na watoto wao Rumisha Msuya kutunukiwa Degree yake ya kwanza na Ngazo Msuya kuapishwa kuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Neno: Zaburi 138:1-3, Wimbo: TMW 104

6. NDOA ZA WASHARIKA

MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 30/12/2023 

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT- KANISA KUU AMANI MWANZA KATI YA

  • Bw. Goodluck Manota Dalali na Bi.Elizabeth Jeremiah Mohamed

MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 16/12/2023 

SAA 08:00 MCHANA

  • Bw. Wilbert Exaud Kwayu na Bi. Simona Mrinji Gadi 

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. James Modest Mero na Bi. Vicky Kawedi Shayo

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

7. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa ………………………..
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa …………………………..
  • Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi Kulaba
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………………..
  • Upanga: Kwa Bi. Agnes Mziray
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………………

8. Zamu: Zamu za wazeeni ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.