MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 24 DISEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA 4 KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

BWANA YU KARIBU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 17/12/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Usharika unapenda kuwatangazia Wazazi na Walezi kuwaandikisha watoto wa Kipaimara Mwaka wa Kwanza 2024 katika ofisi ya Parish Worker. Umri ni kuanzia miaka 12.  

6. Kwaya ya Agape inapenda kuwajulisha washarika kuwa wanajiandaa kutembelea watoto wenye vichwa vikubwa na kuwalipia Bima katika Hosptali ya Taifa Muhimbili Moi kama wafanyavyo kila mwaka kwa Mwezi January. Mwaka jana Washarika mliwawezesha kuwalipia watoto 130 kwa kuwalipia bima ya afya na kununua friji kubwa la kuifadhia vyakula maziwa na dawa. Mwaka huu tunatamani kuwalipia angalau watoto 150. Wanaomba washarika muwaunge mkono kwa kutoa fedha, pampas, sabuni, dawa za meno, maji, juice. Unaweza kuwasilisha kwa Mhasibu wa usharika, Parishi Worker au Mtunza hazina wa agape no: 0767214441 Janice kaisi au Acc No. 013874006021 MAENDELEO BANK Jina AGAPE EVANGELICAL SINGER AZANIA FRONT. Washarika walioamua kulipia watoto 10 kila mwaka wanaombwa wawasiliane na uongozi wa Agape kupata taarifa mpya za NHIF. Mungu awabariki sana. Pia agape wanaendelea kuuza kalenda zao za mwaka 2024.

7. Jumapili ijayo tarehe 31/12/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

8. Uongozi wa Usharika unapenda kuwakumbusha Washarika kulipa madeni ya mavuno ya nyuma ili waweze kukamilisha ahadi zao. Washarika ambao wamesahau madeni yao wafike ofisini kwa Mhasibu.

9. Jumapili ijayo tarehe 31/12/2023 waliozaliwa mwezi Desemba Kwaya Kuu watatoa shukrani ya pekee katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi, pia wanatoa mwaliko kwa Washarika wote waliozaliwa Desemba kuungana nao kumshukuru Mungu kwa mambo Makuu aliyowatendea. Wameandaa bahasha maalum, watakaohitaji wamuone Mzee George Mnyitafu.

10. NDOA ZA WASHARIKA

MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 30/12/2023 

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT- KANISA KUU IMANI MWANZA KATI YA

  • Bw. Goodluck Manota Dalali na Bi.Elizabeth Jeremiah Mohamed

11. RATIBA YA SIKUKUU 

JUMAPILI TAREHE 31/12/2023 

Ibada itakuwepo -

Saa 1.00 asubuhi

Saa 3.00 asubuhi

Saa 4.30 asubuhi

Saa 1.00 usiku; ibada ya Kiswahili kupokea Mwaka Mpya.

JUMATATU TAREHE 01/01/2024 

Ibada zitakuwa 2

Saa 2.00 asubuhi Kiswahili

Saa 6.00 mchana Kingereza.

12. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.