Date: 
18-04-2024
Reading: 
Luka 19:10

Alhamisi asubuhi tarehe 18.04.2024

Luka 19:10

[10] Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Bwana huchunga na kulisha kundi lake;

Zakayo alitaka kumuona Yesu, na kwa sababu alikuwa mfupi aliamua kupanda kwenye mti. Alipanda kwenye mti kwa sababu ya umati, asingemuona Yesu. Mtoza ushuru huyu aliambiwa na Yesu kushuka mtini, akiambiwa wokovu kufika nyumbani kwake.

Zakayo baada ya kumpokea Yesu alitoa nusu ya mali yake kuwapa maskini, na aliokuwa amewadhulumu kuwarudishia mara nne. Yesu akatangaza wokovu katika nyumba ya Zakayo.

Baada ya hapo ndipo unakuja mstari wa somo la asubuhi hii, kwamba Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Yaani ni kuwa Yesu alikuja kuokoa waliopotea kama Zakayo. Zakayo ni alama ya watu watubuo na kumrudia Bwana. Kristo aliye Mchungaji mwema anatualika kuishi maisha ya toba ili tuwe na mwisho mwema. Amina

Alhamisi njema 

Heri Buberwa