Date: 
30-04-2024
Reading: 
Isaya 42:10-13

Jumanne asubuhi tarehe 30.04.2024

Isaya 42:10-13

10 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo.

11 Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima.

12 Na wamtukuze Bwana, Na kutangaza sifa zake visiwani.

13 Bwana atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.

Njooni tumwimbie Bwana;

Taifa la Mungu wakiwa uhamishoni wanapewa ujumbe wa matumaini, kwamba Bwana yuko upande wao. Wanapewa ahadi ya kukombolewa (13) na kwa ahadi hiyo wanaelekezwa kudumu katika ibada wakimsifu Bwana. Ujumbe huu ni kwa watu wote, maana Bwana alitoa ahadi kwa watu wake wote.

Sisi tumeokolewa kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani na kufufuka. Tunapofurahia na kushangilia wokovu huu, tunaalikwa kumsifu Bwana daima. Sifa zetu zinakuwa njema mbele za Bwana pale tunapoishi na kudumu katika imani ya kweli, toba na msamaha. Amina.

Heri Buberwa