Date: 
12-06-2025
Reading: 
Matendo ya Mitume 4:1-4

Hii ni Pentekoste 

Alhamisi asubuhi tarehe 12.06.2025

Matendo ya Mitume 4:1-4

1 Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,

2 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.

3 Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.

4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.

Roho Mtakatifu ni ushindi wetu;

Petro na Yohana wakikwea hekaluni walimkuta kiwete kwenye mlango wa hekalu, naye akiomba kupata kitu kwao. Petro akamuombea uponyaji, akasimama na kutembea katika jina la Yesu. Humo hekaluni Petro akaanza kuhubiri Injili. Watu wengi waliamini. Sasa wakiendelea kuhubiri ndipo tunasoma katika somo la asubuhi hii makuhani na maakida wa hekalu wakitokea. Makuhani hawa walifadhaika kwa sababu waliwasikia Petro na Yohana wakifundisha kuhusu Yesu Kristo. Wakawakamata na kuwaweka gerezani usiku kucha. 

Ukiendelea kusoma unaona wakitolewa gerezani, na mashtaka ya kuwatia hatiani yanakosekana. Petro aliwakabili wajumbe wa baraza kwa msaada wa Roho Mtakatifu;

Matendo ya mitume 8

Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

Nimenukuu mstari mmoja tu bila mwendelezo wake hapo juu ili uone kwamba Petro alijawa na Roho Mtakatifu mbele ya baraza. Petro na Yohana waliishia kutishwa tu na kuachiwa, maana Roho Mtakatifu alikuwa juu yao. Nasi tukiwa na Roho Mtakatifu tunashinda yote. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa