Date: 
02-08-2025
Reading: 
Marko 9:38-44

Jumamosi asubuhi tarehe 02.08.2025

Marko 9:38-44

38 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.

39 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;

40 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.

41 Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.

42 Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini.

43 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;

44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

Mambo yote yatendeke katika upendo wa Kristo;

Wanafunzi walikuwa wamemuona mtu akifanya huduma ya neno la Mungu wakamzuia kwa sababu hakuwa anafuatana na Yesu! Yohana anampa Yesu hiyo taarifa, Yesu anaikosoa taarifa hiyo, kwa sababu mhusika alihudumu kwa jina la Yesu. Kwa mkazo kabisa Yesu anasema asiye kinyume chetu yu upande wetu. Yesu anaendelea kuwasihi wanafunzi wake kutowakosesha wengine katika huduma, maana wote wanahudumu kwa jina lake.

Yohana anapotoa taarifa kwa Yesu kuhusu aliyetoa pepo kwa jina la Yesu, alionesha kwamba yule hakutakiwa kufanya hivyo kwa kuwa hakuwa mwanafunzi wa Yesu! Ubinafsi na kujipendekeza haukuanza leo. Baadhi yetu hujiona tuko karibu na Mungu kuliko wengine! Tunabagua wengine hadi salamu, kuna wanaosalimiwa "Bwana Asifiwe" na wengine "habari ya nyumbani"? Tunajiona tuko karibu na Mungu. Huo ni ubaguzi unaotufanya kuwa karibu na Kanisa, mbali na Mungu. Tupendane. Amina

Jumamosi njema 

Heri Buberwa