Date: 
04-09-2025
Reading: 
Zaburi 10:13-18

Alhamisi asubuhi tarehe 04.09.2025

Anza siku yako hi kwa jina la Yesu.

Zaburi 10:13-18

13 Kwani mdhalimu kumdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?

14 Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.

15 Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione.

16 Bwana ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake.

17 Bwana, umeisikia tamaa ya wanyonge, Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako.

18 Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu.

Muvngu huwapinga wenye kiburi;

Inaaminika kwamba Zaburi ya kumi ni yake Daudi kama alivyoimba, kwa kusoma aina ya mashari yake yalivyo. Pia wapo wasomi baadhi ambao hawaoni tofauti kati ya Zaburi ya 9 na 10, maana zote zinahusika na uwezo wa Mungu na haki yake. Sehemu tuliyosoma Daudi anakataa dharau kwa Mungu akisema ipo adhabu kubwa kwa watu wa namna hiyo. Daudi anasema Bwana ataitegemeza mioyo ya wamchao na kuwahukumu wenye dhambi.

Daudi anakazia kwamba Bwana ndiye Mfalme, hivyo wote watendao yasiyofaa wamepotea kutoka nchi yake! Yaani nchi na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana, hivyo kutomcha ni kupotea katika nchi ya Bwana! Mstari wa 13 unabeba ujumbe wa leo, kwamba wenye dharau, kiburi, jeuri, udhalimu n.k watahukumiwa. Tuache kiburi, tutahukumiwa. Amina

Alhamisi njema.