Jumatano asubuhi 10.10.2025
Luka 18:35-43
35 Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka;
36 na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini?
37 Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.
38 Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.
39 Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.
40 Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,
41 Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.
42 Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.
43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.
Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu;
Yesu anamkuta kipofu kando ya njia akiomba sadaka, kipofu ambaye aliposikia Yesu anapita alipiga kelele akiomba Yesu amrehemu. Waliomzunguka walimkemea lakini yeye ndipo alizidi kupaza sauti. Yesu akamuuliza alitaka nini, yule kipofu akasema nataka kuona. Yesu akamwambia "imani yako imekuponya". Ni tukio ambalo lilifanya aliyeponywa na wote waliomshuhudia kumsifu Mungu.
Tunachoona leo asubuhi ni imani ya kipofu katika Yesu Kristo kwamba angeweza kumponya. Bila shaka alishatibiwa sehemu nyingi, na alikwisha kusikia habari za Yesu. Alitumia fursa, hakutaka kuipoteza. Kwa tafakari ya juma hili, naweza kusema yule ndugu kipofu aliutumia ulimi wake vizuri mbele ya Yesu akapona. Tumia ulimi wako kwa Utukufu wa Mungu. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650