Date:
13-09-2025
Reading:
Yakobo 4:11-12
Jumamosi asubuhi tarehe 13.09.2025
Yakobo 4:11-12
11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu;
Yakobo anaandika kwa ufupi akionya juu ya kumhukumu mwingine. Anawasihi waaminio wasisingiziane, maana amsingiziaye ndugu yake au kumhukumu huisingizia sheria. Hii ni kwa sababu sheria ndiyo hutoa haki. Kumhukumu mtu pia ni kuihukumu sheria. Yakobo anasema mwenye kuhukumu ni mmoja tu, maana ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza, Mungu mwenyewe
Yakobo anatukumbusha kama kundi la waaminio kuishi kwa pamoja kwa upendo, maana pasipo upendo ndiyo kunatokea kusingiziana na kuhukumiana. Upendo ukitawala tunaelekezana na kufundishana, hatuhukumiani na kusingiana. Kumbe katika kukaa pamoja kama Kanisa la Mungu, tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu pasipo kusingiziana wala kuhukumiana. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650