Date: 
17-09-2025
Reading: 
Luka 16:19-31

Jumatano asubuhi tarehe 17.09.2025

Luka 16:19-31

19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.

20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,

21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Mtendee mema jirani yako;

Leo tunamsoma mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za thamani na kula siku zote kwa anasa. Maskini aliyeitwa Lazaro alikaa mlangoni kwake akitamani kushibishwa na makombo ya yule tajiri. Lazaro huyu alilambwa vidonda na mbwa! Basi ilitokea yule Lazaro akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Tajiri naye akafa na kuzikwa, huko akakumbana na mateso makali.

Yesu alitoa mfano huu unaoonekana kama tukio halisi kufundisha kwamba maisha ya waaminio ndiyo maandalizi ya kuingia uzimani. Pia tunaona kwamba tajiri alisahau kutoa vipawa vyake kwa wahitaji, alimsahau Bwana akaishia motoni. Maskini Lazaro katika umaskini wake alimcha Bwana. Mtendee mema jirani yako ili matendo yako yakaambatane na wewe mara Yesu arudipo. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com