Date: 
07-11-2025
Reading: 
Isaya 57:1-2

Ijumaa asubuhi tarehe 07.11.2025

Isaya 57:1-2

1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya.

2 Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake.

Tunaitwa kuwa wenyeji wa mbinguni;

Somo tulilosoma ni maneno ambayo walipewa Israeli baada ya kuwa wametoka uhamishoni. Isaya anawatahadharisha kwamba pamoja na kuwa wametoka uhamishoni, wawe makini na mienendo yao. Isaya anawaambia kwamba unaweza kujiona mwenye haki ukaacha kusimama katika Bwana, ukaishia kupotea. Isaya anaendelea kuwakemea akiwasihi kumtazama Bwana, maana kinyume na hapo wao siyo kitu;

Soma hapa;

Isaya 57:4-5

4 Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo;
5 ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi; ninyi mnaoua watoto mabondeni, chini ya mianya ya majabali?

Ujumbe wa Isaya kwa Israeli ulikuwa kumcha Bwana hata baada ya kuwa wametoka uhamishoni. Ujumbe huu unatujia sisi ukitutaka kutomuacha Kristo Yesu kama tulivyompokea pale tulipokiri ahadi ya ubatizo. Kwa kukiri ahadi hiyo, tumetolewa utumwani. Tusiiache imani. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com