Date:
03-12-2025
Reading:
Warumi 13:11-14
Hii ni Advent;
Jumatano asubuhi tarehe 03.12.2025
Warumi 13:11-14
11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
Bwana mwenye haki analijia Kanisa lake;
Paulo anawaandikia Warumi kuutambua wakati, kwamba saa ya kulala usingizi imekwisha. Ni saa ya wokovu. Paulo anawaambia kwamba usiku umeendelea, mchana umekaribia, anawasihi kuyavua matendo ya giza na kuzivaa silaha za nuru. Wito unatolewa wa kuenenda kwa adabu, si kwa ulafi na ulevi, ufisadi wala uasherati, ugomvi au wivu.
Paulo anawaita Warumi kuuacha uovu na kumvaa Bwana Yesu Kristo pasipo kuuangalia mwili wenye tamaa. Ujumbe wa Paulo ulihusu kugeuka na kumtazama Kristo, maana ipo siku atarudi, ndiyo maana Paulo anaonesha kwamba wakati unasogea sana. Ni kweli, wakati haupo, tuangalie njia zetu na kutengeneza maisha yetu maana Bwana mwenye haki analijia Kanisa lake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
