Hii ni Advent;
Jumatano asubuhi 10.12.2025;
Luka 1:67-75
67 Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,
68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.
69 Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
70 Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu;
71 Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
72 Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;
73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,
74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,
75 Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote.
Changamkeni Mkombozi yu karibu;
Zakaria alikuwa Kuhani, siku moja akifukiza uvumba hekaluni akapokea ujumbe toka kwa malaika kwamba atamzaa mtoto, Yohana. Elizabeth mke wake alipata mimba akamzaa mtoto, wakamuita Yohana. Yohana huyu alitangulia kuleta ujumbe wa ujio wa Yesu Kristo, yaani alikuja kuwaandaa watu kumpokea Mesiya.
Baada ya Yohana kuzaliwa, somo linaonesha Zakaria akisema kwa uhakika kuwa Mungu wa Israeli amewajia watu wake kuwakomboa. Analiona agano la Mungu kuokoa watu wake, kama alivyomwapia Ibrahimu. Agano la Mungu lilitimia kwa Yesu kuja kama ilivyosemwa na Yohana mtangulizi wake. Hiyo inatupa uhakika kuwa Yesu atarudi tena kulichukua Kanisa, sasa jiandae ili akirudi asikuache. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
