Event Date: 
12-08-2022

Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral hivi karibuni walihudhuria semina ya kiroho na kiuchumi. Semina hiyo ya siku moja ilifanyika tarehe 30/4/2022 katika kituo cha Consolata Mission Centre, Bunju Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya washarika wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral.

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuwaweka wanawake pamoja kwa ajili ya kupata mafundisho ya kiroho na kiuchumi, iliandaliwa na viongozi wa Umoja wa wanawake usharikani wakishirikiana na uongozi wa Usharika.

Wanawake hao wakiwemo walezi wa umoja wa wanawake usharikani, wazee wa kanisa wanawake usharikani, viongozi wa umoja wa wanawake katika mitaa inayotunzwa na usharika, mitaa ya Dondwe, Mvuti na Tabora pia waliweza kupata mafunzo ya ujasiriamali wa ufugaji wa nyuki na samaki. Pia washiriki wa semina hiyo walipata mafunzo ya uwekezaji katika masoko ya fedha na jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo. Pia mafunzo juu ya nguzo za maisha na masomo yaliyohusu malezi ya watoto na vijana yalitolewa.

-------------------------------

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa semina ya neno la Mungu kwa wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Semina hiyo iliandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral.