Date: 
30-07-2022
Reading: 
1Yohana 4:19-21

Jumamosi asubuhi tarehe 30.07.2022

1 Yohana 4:19-21

[19]Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.

[20]Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

[21]Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.

Amri mpya nawapa, Mpendane 

Asili ya upendo ni Mungu mwenyewe, tangu uumbaji na jinsi alivyokuwa na watu wake, kumtuma Yesu Kristo aje duniani hadi kutuachia Roho Mtakatifu. Mungu yuko nasi hata leo. Hivyo tukipendana twaiga mfano wake. Na katika kupendana huko, sisi tunaoishi pamoja tusipopendana hatuwezi kusema tunampenda Mungu! Huo ni uongo! Unamchukiaje unayemuona halafu umpende usiyemuona? Na ameshasema mpende jirani yako? Mpende adui yako?

Kanisa la Mungu lazima limwabudu Mungu kwa pamoja. Sasa hatuwezi kumwabudu kama hatupendani maana tunaabudu wote. Umoja wetu wa upendo unatufanya tumwabudu Mungu katika kweli. Kupendana ni agizo, ni amri. Tupendane sisi, ndipo upendo wetu kwa Mungu utakuwa ni wa kweli. 

Jumamosi njema.