Date: 
30-11-2022
Reading: 
Luka 17:20-24

Hii ni Advent;

Jumatano asubuhi tarehe 30.11.2022

Luka 17:20-24

20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;

21 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.

22 Akawaambia wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana wa Adamu, msiione.

23 Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate;

24 kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Wayahudi walikuwa wanamsubiri Mesiya ambaye angekuja kurejesha ufalme wa Israeli toka mikononi mwa Warumi. Walipomuuliza Yesu kuhusu ufalme, walitegemea jibu tofauti na walilopewa, maana badala ya kuambiwa utawala wa Warumi ungeisha lini, waliambiwa waache kuchunguza maana ufalme wa Mungu ulikuwa ndani yao.

Yesu aliyekuwa akiwajibu Mafarisayo, alimaanisha kuwa yeye ndiye mwenye ufalme wa Mungu, maana yake walitakiwa kumwamini yeye. 

Tunaupata ufalme wa Mungu tukimwamini na kumfuata. Ahadi yake ni kurudi kwa mara ya pili, hivyo tujiandae kwa ujio wake kwa kumpokea maishani mwetu. 

Uwe na siku njema.