Date: 
17-12-2021
Reading: 
Luka 4:3-6

Hii ni Advent 

Ijumaa asubuhi tarehe 17.12.2021

Luka 3:4-6

4 kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

5 Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;

6 Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.

  • Itengenezeni njia ya Bwana;

Ni tafakari endelevu juu ya Yohana akitangazia watu kujiandaa kumpokea Yesu, wakisafisha mioyo yao. Upekee wa leo asubuhi ni hitimisho kwenye somo, kuwa wote wenye mwili watamwona Bwana.

Wote wanaosafisha mioyo yao kumpokea Yesu watamwona Bwana atakapokuja. Mimi na wewe tutafakari kama kweli njia zetu ziko sawa mbele za Mungu, kiasi kwamba Yesu akirudi tutaingia uzimani.

Siku njema.