Date: 
15-12-2022
Reading: 
Marko 6:14-16

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 15.12.2022

Marko 6:14-16

[14]Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa kutangaa, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake.

[15]Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii.

[16]Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohana, niliyemkata kichwa, amefufuka.

Bwana anawafariji watu wake;

Yesu alikuwa tayari hudumani, lakini Herode alisema mwenye nguvu ni Yohana, amefufuka. Kumbuka Herode alikuwa tayari amemkata kichwa Yohana kwa sababu Yohana alimwambia Herode kuwa alimuoa shemeji yake hivyo ndoa yake ilikuwa batili. Herode hakuamini kama ni Yesu aliyemsikia akitenda kazi.

Herode aliambiwa ukweli na Yohana, badala ya kuufanyia kazi ukweli ule, akamfanyia kazi Yohana! Huu ni uovu mkubwa sana. Jenga tabia ya kusikiliza na kujisahihisha.

Lakini pia Herode bado hakuamini kama yule aliyemsikia akitenda kazi kwa nguvu ni Yesu Kristo! Bado unao wasiwasi kwamba Yesu ni Mwokozi wetu? Huyu ndiye tunayepashwa kuandaa mioyo yetu kumpokea, maana anakuja kulichukua Kanisa.

Siku njema.