Date: 
19-10-2021
Reading: 
Mathayo 13:31-32 (Matthew)

JUMANNE TAREHE 19 OKTOBA 2021, ASUBUHI.

Mathayo 13:31-32

31 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;

32 nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kukaa katika matawi yake.

Njia ya ufalme wa Mungu;

Yesu anatoa mfano wa punje ya  haradali ilivyo ndogo, lakini ikipandwa humea, hukua na kuwa kubwa kuliko mboga zote, hadi kuwa kivutio kwa ndege wa angani kutua juu yake.

Yesu anatuita kuuacha ulimwengu. Tusiangalie uzuri na wingi wa vitu vya duniani, bali kumtazama yeye aliye mwokozi wetu. Matokeo ya kumfuata Yesu ni makubwa, yaani uzima wa milele.

Siku njema.


TUESDAY 19TH OCTOBER 2021, MORNING

The Parables of the Mustard Seed and the Yeast

31 He told them another parable: “The kingdom of heaven is like a mustard seed, which a man took and planted in his field. 32 Though it is the smallest of all seeds, yet when it grows, it is the largest of garden plants and becomes a tree, so that the birds come and perch in its branches.”

Read full chapter

The way to the kingdom of God;

Jesus told the parable of the mustard seed, when it is sown, it grows and becomes larger than all the vegetables, until it becomes a tree, and an attraction for the birds of the air to land on it.

Jesus is calling us not to dwell on the world. Let us not look at the beauty and abundance of the things of the world, but look at Him who is our Saviour. The rewards of following Jesus are great, that is, eternal life.

Good day.