Date: 
17-08-2022
Reading: 
Mathayo 13:44-45

Jumatano asubuhi tarehe17.08.2022

Mathayo 13:44-45

[44]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.

[45]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;

Hekima ituingizayo mbinguni;

Sura ya 13 ya Injili ya Mathayo kwa sehemu kubwa (mst 1-50) ni Yesu akifundisha kwa mifano. Sehemu tunayosoma asubuhi hii ni mfano wa mtu aliyeona hazina nzuri katika shamba akaitamani na kulinunua shamba lile. Pia kuna mfano wa mfanyabiashara aliyeiona lulu nzuri yenye thamani, akatafuta fedha akainunua. Ni mifano inayoonesha watu waliotamani vitu vizuri wakaweka juhudi hadi kuvipata.

Hatma ya maisha yetu katika Imani ni kuurithi uzima wa milele. Tunautamani uzima huo?

Bila shaka jibu ni "ndiyo" kwa kila mmoja wetu. Sasa tuweke jitihada ili kuurithi uzima huo. Jitihada hizo ni kuongozwa na neno la Mungu, tukiishi na kutenda tunavyopashwa kufanya. Tukae kwa Yesu maana yeye hutupa hekima ituingizayo mbinguni.

Uwe na Jumatano njema.