Date: 
23-12-2021
Reading: 
Mika 5:2-5

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 23.12.2021

Mika 5:2-5

2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
 
3 Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.
 
4 Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.
 
5 Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtaondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.

Bwana yu Karibu;

Leo asubuhi tunamsoma Nabii Mika akitabiri kuzaliwa kwa Yesu katika Bethlehemu. Kumbuka Yusufu aliondoka Nazareti ya Galilaya, akaenda kwenye sensa huko Bethlehemu kwenye mji wa Daudi, ambako Yesu alizaliwa, unabii ukatimia.

Hii inaonesha utimilifu wa ahadi za Mungu. Pamoja na kuwa Yusufu na Mariamu walitokea Nazareti ya Galilaya, Yesu alizaliwa kama ilivyotabiriwa huko Bethlehemu.

Vivyo hivyo kama alivyoahidi kurudi, ni kweli atarudi kama mfalme. Sasa umejiandaaje na kurudi kwake? 

Alhamisi njema.