Date: 
05-01-2024
Reading: 
Warumi 8:31

Ijumaa asubuhi tarehe 5/01/23

Warumi 8:31

31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

Tuanze yote katika jina la Yesu Kristo.

Tumwamini Mungu wetu kwa imani kuu, kwani hakuna aliye juu yake. Tujue na tuamini kwamba atatusaidia kushinda majaribu ya maisha yetu. Neno hili linatusaidia kuwa na amani kuwa katika vita yetu tunaye jemadari wa vita.

Siku njema,

Mzee C. Swai