Date:
06-08-2025
Reading:
Wakolosai 1:9-12
Jumatano asubuhi tarehe 06.08.2025
Wakolosai 1:9-12
9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;
10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
11 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
12 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.
Tunaitwa kuzaa matunda mema;
Mtume Paulo anaanza kuandika barua yake kwa watu wa Kolosai kwa kuwapongeza na kumshukuru Mungu kwa ajili yao, kwa jinsi walivyopomkea Yesu Kristo na kudumu katika ushirika kama kundi la waaminio. Anawasihi kudumu katika Injili waliyohubiriwa wakijawa tumaini katika Bwana, bila kusahau kumzalia Mungu matunda katika utume ambao walipewa walipoamini.
Somo tulilosoma ni mwendelezo wa shukrani za Paulo kwa Mungu, kwamba haachi kuwaombea ili wajazwe maarifa ya Mungu na hekima katika safari yao ya imani. Katika sala hiyo, Paulo anawasihi Wakolosai kuenenda wakimpendeza Bwana kwa kuzaa matunda na kuzidi katika maarifa ya Mungu. Anaendelea kuwasihi wamshukuru Mungu aliyewapa wokovu na kuwaingiza katika nuru yake. Wito wa Paulo kwetu asubuhi hii ni kutenda kama ulivyo wajibu wetu kwa Bwana tukimzalia matunda. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650