Date: 
24-05-2022
Reading: 
Yohana 15:16-17

Jumanne asubuhi tarehe 24.05.2022

Yohana 15:16-17

16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

17 Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.

Ombeni katika jina la Yesu Kristo nanyi mtapewa;

Yesu alikuwa akifundisha juu ya mamlaka yake, kwamba yeye ndiye aliye juu ya dunia yote na wanadamu. Ndiye aliyewatuma wamtumikie. Na kwa maana hiyo, katika utume wao huo aliowaita na kuwatuma wafanye, wamwombe yeye kwa jina lake.  

Hivyo nasi leo katika utume wetu tunaalikwa kumtegemea na kumwomba yeye Yesu Kristo, naye atatujibu ili tuweze kuitenda kazi yake aliyotutuma. Kwa maana nyingine, Kristo anatualika kumuomba yeye, ili kazi zetu ziweze kufanikiwa.

Siku njema.