Date:
02-02-2026
Reading:
Mithali 9:1-6
Jumatatu asubuhi tarehe 02.02.2026
Mithali 9:1-6
1 Hekima umeijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba;
2 Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia.
3 Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana,
4 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
5 Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya.
6 Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.
Neema ya Mungu yatuokoa;
Suleimani anaadika juu ya hekima katika kitabu cha kwanza (sura ya 1 hadi ya 9) . Katika sura ya tisa kama tulivyosoma anatumia lugha ya hekima kuita walio wajinga, waliopungukiwa akili. Hekima anawaita wajinga wauache huo ujinga, wakaishi na kuenenda katika ufahamu. Msisitizo wa Suleimani ni ule ule, kwamba kumcha Bwana ndiyo chanzo cha maarifa, na kumjua Mtakatifu ni ufahamu (10).
Asubuhi ya leo tunakumbushwa hekima ya Mungu, kwamba hekima ya kweli ni kumpokea Yesu ambaye ametuokoa bure, kwa neema. Basi tuombe neema hii isiondoke kwetu, ili maisha yetu yawe yenye kumcha Bwana maana hicho ndicho chanzo cha maarifa hapa duniani. Ni kwa neema ya Mungu tunaweza yote. Basi tusiiache imani hii, yaani tusimuache Yesu aliyetuokoa kwa neema. Amina
Uwe na wiki njema yenye neema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
