Date: 
20-05-2022
Reading: 
1 Nyakati 16:23-27

Ijumaa asubuhi tarehe 20.05.2022

1 Mambo ya Nyakati 16:23-27

23 Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

24 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.

25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

26 Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.

27 Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.

Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana;

Daudi baada ya kumtolea Bwana sadaka ya kuteketezwa alimsifu Mungu. Ndipo akawaambia watu wote kumsifu Mungu kama tulivyosoma. Anawasihi kumhubiri Bwana kwa watu wote maana ndiye astahiliye kusifiwa.

Tunakumbuka kumsifu Bwana?

Tunampa heshima?

Tunawajibika kumtolea sadaka Bwana kama Daudi alivyofanya, lakini zaidi ya hapo kumsifu na kumwadhimisha patakatifu pake. Daudi anakazia akisema;

1 Mambo ya Nyakati 16:29-30

29 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;

30 Tetemekeni mbele zake, nchi yote.

Hivyo tunaalikwa kumwabudu Bwana, tukimsifu kwa uzuri wake, maana anastahili. Sifa zetu zitangaze ukuu wake, tukidumu kwake katika imani.

Siku njema.