Date: 
28-11-2023
Reading: 
1 Petro 5:8-11

Jumanne asubuhi tarehe 28.11.2023

1 Petro 5:8-11

8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.

11 Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Maandalizi kwa uzima wa milele;

Petro anaandika juu ya maandalizi ya uzima wa milele kwa kuwaasa wasomaji wake kuwa na kiasi na kukesha, maana Ibilisi huzunguka akitafuta kuharibu Taifa la Mungu. Hapa Petro anamaanisha kuwa maisha yenye uchaji mbele za Mungu humpinga huyo Ibilisi. Petro anaendelea kusema kuwa Mungu aliyewaita watu wake atawatunza wakimwamini na kumtegemea, hata waurithi uzima wa milele.

Hoja ya Petro asubuhi hii ni maisha ya waaminio kuwa katika ushirika na Kristo. Kiasi na kukesha ni kutenda inavyopasa kwa msaada wa Mungu, na kutotoka katika njia ya Bwana maishani. Maandalizi ya uzima wa milele tunayafanya kwa kumwamini na kumuishia Bwana siku zote za maisha yetu. Amina.

Jumanne njema.

Heri Buberwa