Date: 
16-03-2024
Reading: 
Nehemia 12:40-47

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 16.03.2024

Nehemia 12:40-47

40 Ndivyo walivyosimama mikutano miwili yao walioshukuru nyumbani mwa Mungu, na mimi, na nusu ya mashehe pamoja nami;

41 na makuhani, Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania, wenye baragumu;

42 na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, wenye Yezrahia kuwa msimamizi wao.

43 Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi; hata ikasikiwa mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu.

44 Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika.

45 Wakauangalia ulinzi wa Mungu wao, na ulinzi wa kutakasika, na hao waimbaji na mabawabu vile vile, sawasawa na amri ya Daudi, na ya Sulemani mwanawe.

46 Kwa kuwa siku za Daudi zamani, Asafu alikuwa mkuu wa waimbaji, na juu ya nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu.

47 Na Israeli wote, siku za Zerubabeli, na siku za Nehemia, walitoa sehemu za waimbaji na mabawabu, kama ilivyohusika kila siku; nao wakawatakasia Walawi; na Walawi wakawatakasia wana wa Haruni.

Furahini katika Bwana siku zote;

Sura ya 12 ya Kitabu cha Nehemia inatufundisha umuhimu wa kufurahi na kushukuru, tukijitoa kwa ajili ya Bwana. Somo linaonesha jinsi watu walivyotoa dhabihu nyingi kwa furaha kuu waliyokuwa nayo kwa sababu ya Bwana. Kilele cha matoleo kilichochewa na jinsi Walawi na Makuhani walivyotumika.

Furaha iliwafanya watu wamtolee Mungu.

Kwa nini tusimfurahie Kristo kwa wokovu aliotupa na kujitoa kwa ajili yake? Kujitoa siyo kwa matoleo tu, bali mfumo wetu wote wa maisha kuwa kwa Utukufu wa Mungu. Tutubu na kurejea kwa Bwana ili furaha ya Kristo idumu ndani yetu, sasa na hata milele. Amina.

Tunakutakia Jumamosi njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri