MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 14 APRILI, 2024

SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

 BWANA HUCHUNGA NA KULISHA KUNDI LAKE 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 07/04/2024

Jumla - Tshs 23,790,500/= USD 300/= 

4. MATOLEO KATIKATI YA WIKI 

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaomba wazazi kuwa watoto wataanza mazoezi ya nyimbo za tamasha ambalo litafanyika mwezi wa tano. Hivyo zoezi litaanza jumamosi ijayo tarehe 20/04/2024 saa 6.00 mchana mpaka saa 8.00 mchana. Mungu awabariki wazazi kwa utayari wenu kwa kuwaruhusu watoto. 

7. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 21/04/2024 

KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI.

  • Familia ya Bwana na Bibi Isack Baha wanamshukuru Mungu kwa Baraka ya Mtoto wao Shireen anayeadhimisha Mwaka mmoja tarehe 21/04/2024. 

Neno Isaya 54:13, Wimbo No. 391.

KATIKA IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI.

  • Neema Linda Cornelio pamoja na familia watamshukuru Mungu kwa Kustaafu kazi baada ya kutimiza umri wa miaka 60 pamoja na mambo mengi makuu aliyomtendea.

Neno: Wafilipi 4:6, Wimbo: TMW 295

8. NDOA: HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao karibu na duka letu la vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Mama Ndossi- Mtaa wa Kirombero
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw na Bibi Charles Lyimo
  • Kinondoni: Watatangaza
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana Godfrey Monyo. 
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Oysterbay, Masaki: Watatangaza

10. Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.