Date: 
19-03-2024
Reading: 
Mathayo 5:21-24

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 19.03.2024

Mathayo 5:21-24

21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;

Tunaisoma hotuba ya mlimani kwa sehemu, Yesu akifundisha juu ya maagizo ya kale, na maelekezo yake kama utimilifu wa torati. Mstari wa 21 Yesu anarejea amri ya kutoua, lakini anasema siyo kuua tu, hata kumwonea hasira ndugu yako haitakiwi. Yesu anakazia kupatana kwanza na ndugu kabla ya kupeleka sadaka.

Yesu anaonesha kwamba yeye ndiye alikuja kuitimikiza torati;

Mathayo 5:17

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

Kumbe wokovu wetu ni kwa njia ya Yesu Kristo, pale alipokufa na kufufuka kwa ajili yetu. Hatuko chini ya sheria, bali neema yake hutuwezesha. Upatanisho wa kweli uko kwa Yesu, tumwamini yeye daima. Amina.

Jumanne njema

Heri Buberwa