Date: 
26-11-2021
Reading: 
Yeremia 31:14-17

Ijumaa asubuhi 26.11.2021

Yeremia 31:14-17

[14]Nami nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono, na watu wangu watashiba kwa wema wangu, asema BWANA

[15]BWANA asema hivi, 

Sauti imesikiwa Rama, 

kilio, na maombolezo mengi, 

Raheli akiwalilia watoto wake; 

asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako,

[16]BWANA asema hivi, 

Zuia sauti yako, usilie, 

na macho yako yasitoke machozi; 

Maana kazi yako itapata thawabu, 

nao watakuja tena toka nchi ya adui; 

Ndivyo asemavyo BWANA.

[17]Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema BWANA; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Nabii Yeremia alikuwa anatoa ujumbe juu ya Israeli kurejea kwa shangwe kutoka kuwa mateka, akiwapa ujumbe wa kutokuomboleza maana BWANA ndiye faraja kwao. Anahitimisha kuwa liko tumaini kwa siku za mwisho, ambapo Mungu atawapa haja zao.

Wakati mwingine maisha tunayoishi ni kama tuko Babeli, tumetekwa. Ni ahadi ya Mungu kutukomboa na kuturejesha kwake. Anatupa tumaini la uzima kuelekea mwisho wetu. Baada ya shida zote, Bwana atatupa uzima wa milele. Tudumu tukitenda mema tukiiendea mbingu, katika uzima wa Ulimwengu ujao.

Siku njema.