Date: 
18-07-2022
Reading: 
1Samwel 3:1-4

Jumatatu asubuhi tarehe 18.07.2022

1 Samweli 3:1-4

[1]Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.

[2]Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),

[3]na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu;

[4]basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.

Tunaitwa kuwa wanafunzi na wafuasi;

Samweli aliitwa na Mungu lakini hakutambua, akamwendea Eli mara tatu zote alizoitwa. Eli alitambua kuwa Samweli aliitwa na Mungu, akamwambia akiitwa aseme "nena Bwana kwa kuwa mtumishi wako anasikia". Samweli alikuwa anapewa ujumbe, kuwa Mungu angeihukumu Israeli kwa sababu ya uovu.

Mungu alimuita Samweli kwenye utume na kumtuma kwa Taifa lake. Vivyo hivyo, leo Yesu anatualika kudumu katika ufuasi wetu kwake kama tulivyoitwa. Ufuasi wetu utakuwa imara kama tutaendelea kujifunza kwa Yesu, ndiyo maana tunaitwa kuwa wanafunzi na wafuasi.

Nakutakia wiki njema yenye ufuasi na uanafunzi kwa Kristo Yesu.

Amina.