Date: 
22-01-2022
Reading: 
1Wakorintho 7:10-11

Jumamosi asubuhi tarehe 22.01.2022

1 Wakorintho 7:10-11

10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

Mungu hutakasa nyumba zetu;

Mungu anatuagiza kuishi viapo vyetu vya ndoa, kwa wenye ndoa takatifu. Ndoa takatifu hufungwa na Mungu mwenyewe, hivyo kutii maagizo ya Mungu katika ndoa ni wajibu wa kila mmoja.

Ndoa ni chanzo cha familia. Hivyo ndoa yenye ushuhuda mzuri ni msingi wa familia bora. Tunawajibika kutafakari juu ya mienendo ya ndoa zetu, na ustawi wa ndoa zetu kwa ujumla. Ndoa yenye msingi wa neno la Mungu hukaribisha baraka za Bwana.

Siku njema.