Date: 
23-09-2022
Reading: 
6 Wakorintho 9:6-9

Ijumaa asubuhi tarehe 23.09.2022

2 Wakorintho 9:6-9

6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.

Uwakili wetu kwa Mungu;

Mtume Paulo anawaonesha Wakorintho faida ya kumtumikiaa Mungu, akifananisha na apandaye haba kuvuna haba, apandaye kwa ukarimu kuvuna kwa ukarimu. Paulo anawasisitiza Wakorintho kutenda walivyokusudia, maana Mungu huwapenda wamtoleao kwa moyo. Kumbe Mtume Paulo alikuwa akiwafundisha kumtolea Mungu kwa moyo.

Apandaye haba huvuna haba. Imani thabiti hutuweka kwa Yesu wakati wote na kutupa hatma njema. Tutende kama tunavyoagizwa na Yesu, maana yeye hupenda wanaomsikiliza. Agizo mojawapo ni kumtolea kwa moyo. Yeye atatujaza neema na kututunza daima.

Alhamisi njema.