Date: 
23-03-2018
Reading: 
Exodus 10:21-29 (Kutoka 10:21-29)

FRIDAY  23RD MARCH 2018 MORNING                               

Exodus 10:21-29       New International Version (NIV)

The Plague of Darkness

21 Then the Lord said to Moses, “Stretch out your hand toward the sky so that darkness spreads over Egypt—darkness that can be felt.” 22 So Moses stretched out his hand toward the sky, and total darkness covered all Egypt for three days. 23 No one could see anyone else or move about for three days. Yet all the Israelites had light in the places where they lived.

24 Then Pharaoh summoned Moses and said, “Go, worship the Lord. Even your women and children may go with you; only leave your flocks and herds behind.”

25 But Moses said, “You must allow us to have sacrifices and burnt offerings to present to the Lord our God. 26 Our livestock too must go with us; not a hoof is to be left behind. We have to use some of them in worshiping the Lord our God, and until we get there we will not know what we are to use to worship the Lord.”

27 But the Lord hardened Pharaoh’s heart, and he was not willing to let them go. 28 Pharaoh said to Moses, “Get out of my sight! Make sure you do not appear before me again! The day you see my face you will die.”

29 “Just as you say,” Moses replied. “I will never appear before you again.”

We read about the struggles of the Israelites as they are seeking to escape from slavery in Egypt. Pharaoh did not want them to leave. But finally God gave them victory and Moses was able to lead them out of Egypt.

As Christians we face many challenges in this life. But Jesus has promised to be with us and help us. Don’t give up keep trusting in Jesus. He will give you victory.

IJUMAA TAREHE 23 MACHI 2018 ASUBUHI                                 

KUTOKA  10:21-29

20 Lakini Bwana akaufanya ule moyo wa Farao uwe mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa waende zao. 
21 Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. 
22 Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu; 
23 hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao. 
24 Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi. 
25 Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia Bwana Mungu wetu dhabihu. 
26 Makundi yetu pia watakwenda pamoja nasi; hautasalia nyuma hata ukwato mmoja; kwa maana inampasa kutwaa katika hao tupate kumtumikia Bwana, Mungu wetu; nasi hatujui, hata tutakapofika huko, ni kitu gani ambacho kwa hicho inatupasa kumtumikia Bwana. 
27 Lakini Bwana akaufanya kuwa mgumu moyo wa Farao, asikubali kuwapa ruhusa waende zao. 
28 Farao akamwambia Musa, Nenda zako, ujiangalie, usinione uso tena; kwani siku hiyo utakayoniangalia uso wangu utakufa. 
29 Musa akasema, Umenena vema; mimi sitakuangalia uso wako tena.

Hapo juu tunasoma jinsi Waisraeli wanahangaika kupata ruhusa kuondoka Misri. Farao alitaka kukataa. Lakini mwishoni Mungu aliwapa ushindi na walitoka Misri wakiongozwa na Musa.

Kama Wakristo tunapata mahaingaiko mengi hapa duniani. Lakini tusikate tamaa. Tumtegemee Yesu Kristo atatupa ushindi.