Date: 
14-03-2023
Reading: 
Isaya 40:26

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi 14.03.2023

Isaya 40:26

Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.

Tutunze mazingira;

Sehemu hii ya unabii wa Isaya iliandikwa wakati ambao Israeli walikuwa uhamishoni. Nabii Isaya alikuwa akiwaita kumtazama Bwana aliyeziumba mbingu na dunia. Isaya anawaambia Israeli kuwa Mungu ndiye mkuu, hodari mwenye nguvu aliye juu ya vitu vyote. Isaya anatumia maneno "Inueni macho yenu juu mkaone..." akiwataka Israeli kumtazama Bwana.

Wito huu unakuja kwetu asubuhi hii, kwamba tumtazame Bwana aliyeumba mbingu na dunia. Yeye yuko juu ya vyote, huvitunza pia. Tunaalikwa kumtazama Bwana kwa kumcha, tukiutunza uumbaji wake. Tukitunza mazingira tunaheshimu uumbaji wake, na dunia inakuwa sehemu salama kwa viumbe vyake. Hima tutunze mazingira.

Jumanne njema 

 

Heri Buberwa