Date: 
20-12-2021
Reading: 
Isaya 52:13-15

Hii ni Advent;

Jumatatu asubuhi tarehe20.12.2021

Isaya 52:13-15

13 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.
 
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
 
15 ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.

Bwana yu Karibu;

Isaya alitabiri ujio wa Yesu Kristo, kama Mungu mwenye utukufu aliye na mamlaka juu ya wafalme wote wa dunia. Isaya alikuwa anaelezea ujio wa Yesu, ambao tunaendelea kukumbushwa kuwa kama alivyokuja mwanzo, atarudi tena.

Tunapoendelea kumngojea Yesu, tufahamu na kuzingatia kuwa ni kweli atarudi. Msisitizo ni uleule, kutengeneza njia zetu ili anaporudi asituache, maana yu karibu sasa.

Uwe na wiki njema.