Date: 
18-11-2021
Reading: 
Kumbukumbu la torati 7:6-11

Alhamisi asubuhi 18.11.2021

Kumbukumbu la Torati 7:6-11

[6]Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.

[7]BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;

[8]bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.

[9]Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu;

[10]naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake.

[11]Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende.

 

Hukumu ya mwisho;

BWANA hakuwapenda Israeli kwa sababu walikuwa wengi. Ukweli ni kuwa wachache. Ilikuwa ni kutimiza ahadi yake kwa babu zao toka alipowachagua, akawakomboa toka utumwani Misri.

Hatuna sifa yoyote ya ziada, ya kwa nini Mungu ametuokoa. Ni kwa sababu ya upendo na uaminifu wake kwetu. Hivyo hatuna budi kuwa waaminifu kwake tukizishika amri zake, maana tutalipwa kwa kadri ya tulivyojitoa kwake na kumwamini. Basi tuzishike sheria zake na kumfuata kwa ukamilifu, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Siku njema.