Date: 
19-10-2016
Reading: 
Luke 18:1-6 New International Version (NIV)

DAILY WORD

WEDNESDAY 19TH OCTOBER 2016  MORNING

{Presented by Pr. Prudence Chuwa}                         

Luke 18:1-6 New International Version (NIV)

The Parable of the Persistent Widow

1 Then Jesus told his disciples a parable to show them that they should always pray and not give up. He said: “In a certain town there was a judge who neither feared God nor cared what people thought.And there was a widow in that town who kept coming to him with the plea, ‘Grant me justice against my adversary.’

“For some time he refused. But finally he said to himself, ‘Even though I don’t fear God or care what people think, yet because this widow keeps bothering me, I will see that she gets justice, so that she won’t eventually come and attack me!’”

And the Lord said, “Listen to what the unjust judge says.

Jesus is teaching us to persevere in prayer. It is good for us to keep praying to God about our own needs and the needs of others. God knows what we need before we ask and He is willing and able to answer our prayers. But we need to come to God daily in humility and recognize that we are not self-sufficient.  We all need God’s help and we need to help and to receive help from other people. 

 

JUMATANO TAREHE 19 OKTOBA 2016 ASUBUHI       

LUKA 18:1-6

1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. 
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. 
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. 
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, 
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. 
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. 
 

Yesu anasisitiza tuwe na bidii katika maombi na tusikate tamaa. Mungu anajua mahitaji yetu kabla ya sisi kuomba, lakini ni kwa faida yetu tunaomba. Tuombe kwa ajili ya mahitaji yetu wenyewe na kwa watu wengine. Tusijivune au kuona kwamba hatuhitaji msaada. Sote tunapaswa kuja kwa Mungu kila siku katika maombi. Pia tunapaswa kusaidia na kuomba msaada kutoka binadamu wenzetu.