MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 11 MARCH, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUTUNZE UUMBAJI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kwamba Jumapili ijayo tarehe 18/03/2018 tutakuwa na ibada ya maombi kwa  Usharika mzima katika ibada zote mbili.  Kwa jinsi hii washarika wanataarifiwa kuandaa mahitaji yao na kuyaandika ili kuwasilishwa madhabahuni siku hiyo.  Tutakuwa na sadaka maalumu ya kusindikiza maombi hayo. Siku hiyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika wote tuiombee siku hiyo.

4. Jumatano ijayo tarehe 14/03/2018 tunaendelea na ibada ya Kwaresma kama kawaida. Washarika wote mnahimizwa kuiadhimisha. Tunaendelea na mafundisho maalumu juu ya "MAMLAKA UWEZA NA NGUVU YA DAMU YA YESU". Mafundisho yatakuwa ni  siku tatu kama kawaida Jumatano, Alhamis na Ijumaa kuanzia saa 11.00 jioni. Jumuia ya  KAWE/MIKOCHENI/MBEZI BEACH itaongoza liturgia ya ibada ya Kwaresma siku ya Jumatano, Kwaya zitakazohudumu ni Kwaya Kuu na Kwaya ya Vijana. Aidha Maombi na Maombezi siku za Alhamisi yataendelea kwa kipindi cha Kwaresma, yakiambatana na mafundisho maalum.

5.Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa yeyote ambaye hakujaza fomu kwa ajili ya namba mpya za bahasha asitumie bahasha yeke aliyokuwa anatumia zamani afike ofisini ili kupata namba mpya.  Kuna baadhi ya Washarika wanatumia namba zao za zamani na kusababisha usumbufu  kwa wengine.

6. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kwamba tarehe 24/03/2018 saa 4.00 asubuhi tutakuwa na ibada maalum itakayoambatana na Chakula cha Bwana kwa washarika wetu wote wenye umri kuanzia miaka 65 na kuendelea.  Pia kutakuwa na maongezi ya pamoja.  Wazee wote hao wanakaribishwa. Tungependa kupata muitikio wa idadi ya watakaoshiriki katika ibada hii.  Kwa  Wazee  ambao watahitaji huduma ya usafiri tunaomba taarifa zao kwenye ofisi ya Chaplain.

7. Jumapili ijayo tarehe 18/03/2018 Sister Elipendo Mkandawire na familia yake watatoa shukrani ya pekee kwa mambo mengi Makuu Mungu aliyomtendea. Ikiwa ni pamoja na kutimiza miaka 70 mwezi huu, kufanya kazi ya Muuguzi/Mkunga kwa miaka 50 bila tatizo lolote tangu mwaka 1967 mpaka Desemba 2016.

Neno: Zaburi 105:1-4, Wimbo: 312 Ubeti wa 1 na wa 5.

8. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Watashiriki semina hapa usharikani

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Alpha Mlenga.

- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watashiriki semina hapa usharikani

- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watashiriki semina hapa usharikani

- Oysterbay/Masaki: Watashiriki ibada hapa usharikani Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa.

- Mjini kati:  Kwa  Bibi Twilumba Talawa

- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa  Dr na Bibi Nangawe

- Tabata:  Kwa ……………………………

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

 

RATIBA YA HUDUMA KATIKA

IBADA ZA JUMATANO KIPINDI

CHA KWARESMA

 

 

TAREHE

 

 

 

JUMUIYA

 

KWAYA INAYOONGOZA

 

 

MTUMISHI

21/02/2018

 

UPANGA  NA  MJINI KATI,

 

KWAYA KUU

 

KWAYA YA VIJANA

 

 

 

 

28/02/2018

 

ILALA/CHANG’OMBE/MIVINJENI,

NA

KINONDONI

 

KWAYA YA UPENDO,

 

KWAYA YA AGAPE

 

 

07/03/2018

 

WANAWAKE

 

KWAYA YA KINAMAMA,

 

TARUMBETA

 

 

14/03/2018

 

KAWE/MIKOCHENI/MBEZI BEACH

 

KWAYA KUU,

 

KWAYA YA VIJANA

 

 

 

21/03/2018

 

OYSTERBAY/MASAKI

NA

KIJITONYAMA/SINZA/MWENGE/

MAKUMBUSHO/UBUNGO

KWAYA YA KINAMAMA,

 

TARUMBETA

 

 

28/03/2018

 

TABATA

NA

WAZO/TEGETA/KUNDUCHI/

BAHARI BEACH/UNUNIO

 

 

KWAYA YA UPENDO

 

KWAYA YA AGAPE

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Viongozi wa vikundi na Jumuiya husika wasimamie utekelezaji wa ratiba hii.