Date: 
27-10-2022
Reading: 
Matendo 14:8-13

Alhamisi asubuhi tarehe 27.10.2022

Matendo ya Mitume 14:8-13

[8]Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa.

[9]Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa,

[10]akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda.

[11]Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.

[12]Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji.

[13]Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng’ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.

Imani yako imekuponya;

Paulo na Barnaba wanaendelea na huduma huko Listra, na huko Paulo anamuona mtu aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Paulo anamuombea na kumuamuru kusimama. Yule kiwete anasimama na kutembea, jambo lililoshangaza wengi. 

Paulo wakati akinena alimuona yule kiwete akiwa mwenye Imani ya kuponywa. 

Maana yake yule kiwete aliamini katika Injili ya Yesu Kristo iliyokuwa ikihubiriwa na Paulo.

Kumbe tukimwamini Yesu anatuondolea shida zetu na kutuwezesha katika yote. 

Yule kiwete alipona kwa Imani.

Nasi tunashinda kwa Imani.

Alhamisi njema.