Date: 
25-10-2022
Reading: 
Matendo 9:32-35

Jumanne asubuhi tarehe 25.10.2022

Matendo ya Mitume 9:32-35

[32]Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida.

[33]Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.

[34]Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.

[35]Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana.

Imani yako imekuponya;

Petro alikuwa akiendelea na utume wake akafika Lida, huko ndipo alikutana na ndugu aliyeitwa Ainea aliyekuwa amelala kwa ugonjwa kwa muda wa miaka nane. Ainea alikuwa amepooza. Petro alimuombea Ainea uponyaji toka kwa Yesu Kristo, na mara akapona.

Haiandikwi kama Petro alitaarifiwa juu ya Ainea mgonjwa, au aliongozwa kumfuata alipo. Mazingira yanaonesha aliwafuata watu wa Lida, akamuona mgonjwa huko. Kupooza kwa kulala kwa miaka nane kuliisha kwa jina la Yesu Kristo. 

Tunapata haja zetu kwa kumtegemea Yesu, tukimfuata kwa Imani. Siku njema