Date: 
13-07-2022
Reading: 
Mathayo 23:13-22

Jumatano asubuhi tarehe 13.07.2022

Mathayo 23:13-22

[13]Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.

[14][Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]

[15]Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.

[16]Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga.

[17]Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu?

[18]Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.

[19]Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka?

[20]Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.

[21]Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake.

[22]Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.

Mungu ni mwingi wa huruma na haki;

Mafarisayo walijiona wenye haki mbele za Mungu wakiishi maisha ya kinafiki. Hawakutenda waliyofundisha! Ndiyo maana ukisoma hii sura ya 23 mwanzoni Yesu anasema wasikilize lakini kwa matendo yao msitende;

Mathayo 23:2-3
[2]Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;
[3]basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.

Sisi tusiwe kama Mafarisayo waliofanya kinyume na waliyoyasema. Tuyaishi tunayoyahubiri. 

Hii ni shida kwa wengi waaminio, kiasi kwamba ni kawaida kukuta mtu aliyebatizwa anatuhumiwa kuiba, kudanganya, kusengenya, kubaka, kuonea wengine n.k Yesu anatuita kutenda yanayostahili kwa Imani yetu. Tuache unafiki, tufanye yanayostahili. 

Siku njema.