Date: 
15-06-2022
Reading: 
Mathayo 3:13-17

Jumatano asubuhi tarehe 15.06.2022

Mathayo 3:13-17

13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.
 
14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
 
15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.
 
16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
 
17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Yesu anabatizwa na Yohana Mbatizaji katika ubatizo wa toba aliouhubiri Yohana. Lakini katikati ya ubatizo huo, utatu Mtakatifu unajitokeza, maana aliyebatizwa ni Yesu mwenyewe, Roho Mtakatifu alimshukia baada ya kubatizwa na sauti ilitoka mbinguni ikisema huyu (Yesu) ndiye mwanangu ninayependezwa naye.

Nasi tunabatizwa na "maji yenye neno la Mungu" katika Utatu Mtakatifu. Kumbe tunabatizwa kwa jina la Mungu wa Utatu. Hivyo tunawajibika kuishi ahadi yetu ya ubatizo, kwa kutenda yatupasayo katika imani kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Siku njema.