Date: 
28-12-2021
Reading: 
Mika 5:1-3

Jumanne asubuhi 28.12.2021

Mika 5:1-3

1 Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
 
2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
 
3 Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.

Stefano shahidi mwaminifu wa Yesu;

Somo la leo asubuhi ni utabiri wa Mika kuhusu Yesu kuja duniani kama mwanadamu. Utabiri huu ulitimia kwa Yesu kuzaliwa Bethlehemu, kama tunavyoendelea kuadhimisha kuzaliwa kwake katika majira haya.

Tunaitwa kumpokea Yesu huyu aliyezaliwa kwa ajili yetu, kwa ajili ya maisha ya sasa na baadae. Yesu akionekana kwetu tunamshuhudia moja kwa moja kwa wengine, na hapo tunakuwa mashahidi wake. Maisha yetu yawe ushuhuda, na hapo ndipo tutakuwa mashahidi wema katika yeye.

Siku njema.