Date: 
17-02-2023
Reading: 
Mithali 4:1-5

Ijumaa asubuhi tarehe 17.02.2023

Mithali 4:1-5

1 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.

2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.

3 Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.

4 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.

5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.

Neno la Mungu lina nguvu;

Asubuhi ya leo tunasoma juu ya kusikia mausia ya Baba. Tunaona juu ya kutega masikio ili kupata ufahamu kwa mafundisho mazuri pasipo kuiacha sheria ya Mungu. Daudi anatoa mfano wake yeye alivyokuwa mtoto, akawasikiliza wazazi wake. Walimfundisha kuyahifadhi mema waliyomfundisha. Vivyo anatoa ujumbe wa kumsikia Bwana.

Muktadha wa somo letu asubuhi ya leo ni kulisikia neno la Mungu ambalo hutupa ufahamu wa kumjua Mungu. Kwa njia ya neno la Mungu tunakutana naye akitufundisha jinsi ya kuishi tukimwamini na kumtumaini yeye. 

Ukiendelea kusoma, Daudi anakazia kwa lugha rahisi akisema;

Mithali 4:20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.

Sauti ya Bwana inatuita kusikia neno lake, maana ndilo lenye ufahamu juu ya Imani yetu.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa